Ebola ni ugonjwa unaohatarisha maisha unaosababishwa na virusi vya Ebola. Kwa sasa hakuna tiba wala chanjo yake. Ingawa ugonjwa huu ni hatari na unaweza kuua katika muda mfupi, tunaweza kuzuia kuenea kwa Ebola. Matibabu ya mapema pia yanaweza kuongeza uwezekano wa kupona Ebola. Video hii inatoa habari kuhusu dalili za Ebola, jinsi inavyoenea, na jinsi tunavyoweza kuizuia kuenea.