Articles


Kilimo hifadhi katika Afrika Mashariki

Erwin Kinsey, Mkurugenzi wa ECHO – Kanda ya Afrika Mashariki

Kilimo Hifadhi (Conservation Agriculture - CA) kimendelezwa katika Afrika Mashariki kwa miaka michache sasa. Katika makala hii, ECHO inashirikisha mbinu zilizopatikana kutoka kwa wana mtandao wa Africa Conservation Tillage Network (ACT) na wadau wengine wenye uzoefu katika nchi mbalimbali za Afrika, ikitumaini kwamba msomaji anaweza kupanua ufahamu wake  juu ya mbinu mpya na mafanikio katika mada hii ya KILIMO HIFADHI. 

Kama ungependa kushirikisha uzoefu wako katika Kilimo Hifadhi au kushiriki katika maswali kwenye tovuti, tazama ECHO Conversations chagua lugha KISWAHILI uende katika ' Vikundi ', bonyeza ' Kilimo Mbinu ', bonyeza ' Kilimo Hifadhi ', na ushiriki!

Telfairia pedata

Telfairia pedata ni zao la asili katika Afrika mashariki na kati . (Aina moja, Telfairia occidentalis inapatikana Afrika Magharibi)  na na mbegu zenye ukubwa wa sentimita 4 na inafanana na shilingi za zamani, na mbegu zake zinakuwa na sifa kama karanga, yaani ina protini nyingi zaidi ya asilimia 30 na mafuta zaidi ya asilimia 60, mafuta ambayo ni mazuri sana kama lishe


mikoa/kanda

East Africa