Limechapishwa: 01-07-2013


Telfairia pedata - inapopatikana na matumizi yake:

EAN oyster nut up closeTelfairia pedata ni zao la asili katika Afrika mashariki na kati . (Aina moja, Telfairia occidentalis inapatikana Afrika Magharibi)  na na mbegu zenye ukubwa wa sentimita 4 na inafanana na shilingi za zamani, na mbegu zake zinakuwa na sifa kama karanga, yaani ina protini nyingi zaidi ya asilimia 30 na mafuta zaidi ya asilimia 60, mafuta ambayo ni mazuri sana kama lishe. Mbegu zinaweza kuhifadhiwa hadi miaka minane bila kuharibika.Huliwa kwa kuchoma, kuchemsha, au kula hata zikiwa mbichi, ladha yake inalinganishwa na nazi. Inafaa sana kuchomwa na kusagwa na kupikwa na samaki au ndizi. Katika jadi za waChagga katika Tanzania ni lishe kwa mama mwenye ujauzito.

Zao hili linasaidia kuongeza maziwa kwa kina mama wanaonyonyesha na vile vile inaongeza uzito kwa jamii. T. pedata si mti bali ni jamii ya matango (Cucurbitaceae). Mimea kike huzalisha maua zambarau na mbegu zake huwana uvimbe (ellipsoid)] na inafikiriwa kuwa una uwezo wa kuchipua na kuzaa kuliko mbegu za mimea dume ambazo ni nyembamba. Mbegu zaidi ya 100 hadi 150 inazaliana ndani ya tunda moja ambalo linafikia  hadi kilo 15. Mbegu zimefungwa kwa namna kama gunia kwa nje, na ndani zina ganda ngumu. Kama vile mzabibu zao hili linakua likipandia mti mwingine hadi urefu wa mita 30 ha hivyo hupenda kutegemeana na mti wenye nguvu.

Kilimo na mavuno

EAN oyster nut fruitHupandwa kwa mbegu katika kina cha sentimita 2.5  na umbali wa sentimita angalau 60.Mbegu huota baada ya wiki mbili au tatu. Kwa sababu mimea ni aidha ya kiume au ya kike (dioecious), ni muhimu kuanzisha mimea ya jinsia zote mbili ili kuhakikisha uzalishaji wa matunda. Katika hekta moja , mimea dume inaweza kutoa mbegu za kiume kwa  mimea kike hadi 200. Mimea inazunguka kama kamba na baada ya mwaka 1 ½ - 2 hutoa maua na matunda. Baada ya kutoa maua, uvunaji inatarajiwa baada ya miezi 4½. Kama zikikomaa, zinaanguka au zinaweza kuondolewa kutoka kwenye kokwa na kuoshwa. Zikiiva, unaweza kukausha mbegu katika jua. Ukikusudia kupanda mbegu, haipaswi kuoteshwa kabla ya kuhifadhiwa kwa muda zaidi ya miezi miwili tokea kuvunwa. Katika mazingira mazuri, inaweza kuzaa kwa misimu miwili kwa mwaka. Mashamba makubwa ya kibiashara yanaweza kufikia wastani wa mavuno wa tani 3 hadi 7 kwa hekta. Mimea inadumu miaka 10 hadi 20. Sehemu kubwa ya uzalishaji katika nchi nyingi ni kwa matumizi ya nyumbani na soko la ndani. Huonekana katika kilimo cha mseto ya Milima ya Meru na Kilimanjaro, ambapo inapandwa katika maeneo yenyemikahawa na migomba.

Vitabu rejea

Rosengarten, Frederic, Jr. The Book of Edible Nuts. pg. 304 Google Books. Web. 09 Apr. 2013. 

Van der Vossen, H.A.M. & Mkamilo. Vegetable oils. pg 164 Google Books. Web. 09 Apr. 2013. 

Orwa C, Mutua A , Kindt R , Jamnadass R, Simons A. 2009. ICRAF Agroforestree Database: A tree reference and selection guide, version 4.0 (http://www.worldagroforestry.org/publication/agroforestree-database-tree-reference-and-selection-guide-version-40)