As made available via the ACT-Africa.org website.   Used by permission.

 

2 Matoleo katika Chapisho hili (Inaonyesha masuala 10 - 4)

Mwongozo wa mafunzo kwa mwezeshaji wa kilimo hifadhi - 20-04-2020

Kilimo hifadhi kimeenea kwa miaka 40 iliyopita hadi kufika hekta milioni 105 za ardhi iliyolimwa duniani kote (ACT 2008). Ufanisi wa kilimo hifadhi katika kuhifadhi unyevu wa udongo, kuboresha udongo, kupunguza gharama za pembejeo,uzalishaji thabiti na mavuno mengi ya mazao kutapelekea kujenga usalama wa chakula katika dunia inayoongezeka idadi ya watu na kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Hata hivyo, kwa bahati mbaya, kupokewa kwa kilimo hifadhi miongoni mwa wakulima wadogo kumebaki nyuma ukilinganisha na wakulima wakubwa wanaotumia zana za kisasa za kilimo. Changamoto kubwa kwa wakulima wadogo kupokea kilimo hifadhi ni tofauti kubwa kati ya ya mazao yanayolimwa na wakulima wadogo pamoja na mbinu na mitazamo tofauti katika maeneo tofauti ya jamii ambapo husababisha kutokuwa na mfumo na kiwango kimoja cha mbinu za kilimo hifadhi. Kwa ujumla, njia, mbinu za huduma ya ugani na vifaa vya ufundishaji hurudisha nyuma kupokelewa na kuenea kwa kilimo hifadhi, hasa dhana ya kuwa suluhisho moja lafaa kwa wote .

Mwongozo wa kilimo hifadhi kwa mwezeshaji umeandaliwa ili kukabiliana na changamoto hizi kwa kujenga kukabiliana na hali tofauti katika kila nyanja ya uzalishaji wa mwongozo na usambazaji. Mbinu na vifaa vinavyotumika ndani ya mwongozo huu zinakubalika katika fani ya kilimo, na, ni rahisi kueleweka kwa wakulima wenye elimu ya msingi . Ni matumaini yetu kuwa uzalisha mwongozo huu katika mfumo wa kielektroniki, bila ya hati miliki kutapelekea ushirikishwa na uboreshaji wa mwongozo na matumizi kwa kila afisa ugani kwa kuzingatia mahitaji, uelewa na mazingira ya eneo husika.

 

Mabango

Kilimo Hifadhi - Kitabu cha Mafunzo ya Wakulima, - 20-04-2020

Kwa Nini Kilimo Hifadhi? ................................................... 3
Kupunguza usumbufu wa udongo ........................................ 5
Umuhimu wa kufunika udongo ............................................ 8
Kupanda kwa usahihi ......................................................... 14
Mazao funika ...................................................................... 16
Kudhibiti magugu na kilimo hifadhi .................................. 22
Usimamizi wa mabaki ya mazao ........................................ 25