uyoga aina ya oyster, shiitake na wood-ear

Agrodok hii inatoa maelezo kamilifu juu ya namna ya kustawisha aina tatu za uyoga-oyster, shiitake na wood ear. Aina hizi za uyoga hasa ni rahisi kustawishwa kwa wakulima wadogo. Kustawisha aina nyinginezo za uyoga kama white button na inayotokana na nyasi za mpunga ni utaalam tofauti sana kwa hiyo kitaandikwa kijitabu tofauti cha Agrodok kwa aina hizo mbili za uyoga wa white button na nyasi za mpunga.

Maelezo yaliyo humu, mengi yamo katika kitabu changu kiitwacho: “Mushroom cultivation and Appropriate technologies for commercial mushroom growers”. Kwa kuchagua aina tatu tu katika maelezo yaliyomo katika Agrodok hii na pia kwa kueleza teknolojia rahisi kwa mkulima, ninatumaini wasomaji watajipatia faida endelevu kwa kustawisha uyoga

Toleo la kwanza kwa kiswahili, 2008