Wakulima huwachukulia viumbe vinavyopunguza mavuno kuwa ni wadudu waharibifu na magonjwa. Wadudu, ndege au wanyama wengine huchukuliwa kama wadudu waharifu wakati wowote ule wanaposababisha uharibifu wa mazao au kwa mavuno yaliyohifadhiwa kwenye ghala. Fangasi, bakteria na virusi hutambulika kama magonjwa, wanapoingilia au kubadili shughuli muhimu za ukuaji wa mimea au mavuno yaliyohifadhiwa. Lakini kimsingi vijidudu vyote ni sehemu ya mfumo asilia, bila kujali wanafanya nini, na wanastahili tuwaheshimu.

 

Kilomohai Training Materials http://www.kilimohai.org/kilimohai/training-materials


mikoa/kanda

East Africa