Je, hifadhi ya mbegu ya ECHO ni biashara au kampuni ya mbegu?

Hapana: ECHO ni shirika lisilo la kiserikali lenye maono ya kumheshimu Mungu kwa kutoa ufumbuzi wa kilimo endelevu, njaa kwa wakulima wadogo na wenye bustani, hasa katika nchi zinazoendelea. Hifadhi ya mbegu ni sehemu ya huduma hii kimataifa. Lengo la hifadhi ya mbegu ni kuwapatia mbegu watu binafsi na mashirika yanayofanya kazi moja kwa moja za kuwasaidia wakulima masikini na bustani; si kutoa mbegu kwa bustani Marekani.

Mimi ni mkulima Marekani, ni kwa jinsi gani naweza kuoda mbegu kutoka ECHO.

Mbegu katika hifadhi ya kimataifa ya mbegu ya ECHO zilizoorodhoshwa zimelenga tu kwa ajili ya wanachama wa nje ya nchi wa mtandao wanaoshiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii. Mauzo binafsi ya mbegu na bustani nchini Marekani yanapatikana kwa njia ya kitabu chi hifadhi cha ECHO na tovuti ya kitabu cha hifdhi.

Wapi ninaweza kupata kiasi kikubwa cha mbegu mnazotoa?

Aina nyingi za mbegu katika orodha yetu zinatoka katika vituo vya utafiti au hifadhi za kimataifa na hazipatikani kwa wingi. Baadhi ya aina zinatokana na tafiti na maonyesho yetu ya kilimo katika Florida. Nyingine zinanunuliwa kutoka katika katika makampuni ya mbegu ya ndani.

Aina gani za mbegu zinaruhusiwa nchini mwangu?

Hii inatofautiana kulingana na nchi na nchi, kulingana na kanuni za nchi za uingizaji. Wasiliana na wizara ya kilimo kwa ajili ya mbegu zilizopigwa marufuku au vikwazo vya aina ya miti. Wakati mwingine mbegu zinaruhusiwa wakati bidhaa za mmea wake haziruhusiwi. Unaweza pia kuwasiliana na hifadhi ya mbegu ya ECHO kwa msaada. Kawaida tupo kwa ajili ya kutupatia msaada unaohitajika.

Je, ninaweza kupata cheti cha usalama?

Tunaweza kukupatia cheti cha usalama kwa ajili ya kusafirisha mbegu kutoka hifadhi ya mbegu kwa ajili ya kusafirishwa, mchakato huu unachukua angalau wiki mbili. Hivyo tafadhali ruhusu muda kwa ajili ya ufungashaji na upatikanaji wa cheti. Mara nyingi ni muhimu kupata kibali cha kuagiza mbegu nchini kabla ya kupata cheti cha usalama. Kama unafikiri unahitaji cheti cha usalama, tafadhali wasiliana na hifadhi ya mbegu moja kwa moja na sisi tutafurahi kukusaidia.  Wasiliana nasi kupitia seeds@echonet.org