Mchicha [Amaranth hypochondriacus, A.cruentus (Nafaka) & A. tricolor (Mboga)] ni mmea unaokua kwa wepesi na imara. Mmea huu hukuzwa kuzalisha nafaka au matawi kutumiwa kama mboga. Matawi na mbegu hutoa proteni nyingi na iliyo ya hali ya juu na ya kipekee. Mbegu husagwa kutoa unga au kupikwa kama popcorn. Malawi yaweza kutumiwa yangali mabichi au hata kupikwa. Ladha ya mchicha wa aina ya mboga ni tamu kuliko ile ya kutoa nafaka. 

Mchicha umekuzwa kwa zaidi ya miaka 8,000, kutoka enzi ya Umayani katika Marekani ya kusini na kati (Mayan civilisation). Riki kilikuwa chakula cha Kidini na chenye manufaa kwa jamii ya Aztecs. Mnamo mwaka wa 1516, Makongwi (conquistadors) walitoa ilani na tahadhari kuu kwamba mchicha usikuzwe. Hadi sasa idadi ya mimea hii ni chache na hutumiwa pamoja na asali kutengeneza "alegria" mfano wa chokoleti. Hata hivyo jamii ya mchicha imedumu tangu jadi na hupatikana kama kwekwe.