Shirikisha uzoefu wako na uvumbuzi huu
Limechapishwa
2025-11-11
ECHO inakusanya mrejesho (maoni) kwenye bunifu nne za kilimo kati ya nyingi zinazofanywa kwa ushirikiano kwenye mtandao wetu wa kimataifa:
- Lishe endelevu – kutumia mazao ya kudumu kama chaya na mlonge kuboresha lishe ya binadamu;
- Kufunga mbegu kwa kutumia pampu ya baiskeli yenye mfumo wa kuvuta hewa (vacuum sealing) kwa ajili ya kuhifadhi mbegu;
- Silaji (chakula cha mifugo) kutoka kwenye mashina ya ndizi; na
- Biochar kwa ajili ya kuboresha udongo na kuhifadhi kaboni.
Maoni yako yatatusaidia kuelewa jinsi ubunifu huu umetumika, umechukuliwa, na kushirikishwa katika muktadha wako.
Utafiti huu unatarajiwa kuchukua takribani dakika 5 kwa kila mada kukamilika. Majibu yako yatatumika kuongoza mafunzo, utafiti, na msaada wa baadaye ndani ya mtandao wa ECHO. Majibu yako pia yanaweza kuchangia katika utafiti unaolenga kuelewa jinsi ubunifu wa kilimo unasambazwa na kutekelezwa katika mazingira mbalimbali. Unaweza kukataa kushiriki au kuacha kujaza dodoso wakati wowote bila adhabu yoyote.
Asante kwa kushirikisha uzoefu wako na kuchangia katika jitihada hizi za kujifunza kwa ushirikiano.