sifa, usindikaji na uuzaji

Nyuki huishi katika makundi, kama ilivyoelezwa kwa undani katika Agrodok 32 – Ufugaji nyuki. Nyuki vibarua katika kundi hukusanya vitu mbalimbali katika mazingira yao kwa matumizi ya kundi hilo, kwa mfano kulisha nyuki waliomo ili kundi liongezeke, au kwa ajili ya kuunda masega au kwa ulinzi wa kundi. Kwa vile nyuki hukusanya vitu vya lishe kutoka kwenye uoto, huwa na umuhimu kwa uoto huo – uchavushaji kati ya mimea ya aina mbalimbali hivyo kuwezesha uundaji matunda bora na utungaji mbegu katika maua ili kutoa matunda na mbegu zilizokomaa.

Version 1, 2005