foodgrainsbank.ca/conservation-a...ure-newsletter/

Wakulima wa mashariki mwa Niger wameweza kukomboa ekari million tano na kuongeza uzalishaji wa chakula kwa zaidi ya tani 500,000 kwa mwaka kwa kutunza miti asilia na vichaka kupitia wakulima kusimamia mali asili. Wakulima kusimamia mali asili ilianza mwanzoni mwa miaka ya 1980,katika miaka ya hivi karibuni imeanza kuenea katika nchi mbalimbali za afrika na zinginezo. Miradi inayowezeshwa na CFGB imeanza kuhusisha wakulima kusimamia mali asili pamoja na kanuni za kilimo hifadhi, zikitambua kua hizo njia mbili zinahusiana.

Ukataji wa miti uliopitiliza nchi ya nusu jangwa Niger katika miaka ya 1950 hadi 1980 ilipelekea hali ya jangwa endelevu, upepo mkali, joto kali na ardhi isiyo na rutuba. Ikijumuishwa na ongezeko la watu kwa kasi zaidi na umasikini uliopelekea kipindi kirefu cha njaa na njaa za muda mfupi. Mamilioni ya dola yalitumika katika njia ya kawaida ya misitu, upandaji wa miti midogo iliyooteshwa kwenye kitalu, lakini ukame, wadudu waharibifu magugu na uharibifu utokanao na binadamu na wanyama vimeacha miti michache ilio hai na athari ndogo sana.

Mwanzoni mwa miaka ya 1980, wakulima pamoja na World vision ilioko Australia wakaanza kutambua kua miti inayofunika ardhi ilikua inaendelezwa upya kwa ubora zaidi kupitia utunzwaji wa mashina ya miti na vichaka vinayobakia baada ya mti kukatwa ambayo bado ipo kuliko kupanda miti mipya kabisa.

Na Neil Miller, Mshauri wa kiufundi wa kilimo na maisha, Mashariki mwa Afrika

Canadian Foodgrains Bank Juni, 2019 JARIDA LA KILIMO HIFADHI