Kitabu cha kuku wa asili

Kuku wa kienyeji ni wale ambao wamekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na damu yao haijachanganyika na ya kuku wa kigeni. Kuku hawa wana rangi na maumbo mbali mbali. Idadi ya kuku wa kienyeji hapa Tanzania inakadiriwa kufikia milioni 27. Kati ya kaya milioni 3.8 zinazojishughulisha na kilimo nchini, kaya milioni 2.3 hujishughulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Ufugaji wa kuku wa kienyeji hapa nchini kwetu Tanzania, kwa kawaida, hufanywa na wafugaji wadogo wadogo wanaoishi kando kando ya miji na wale wanaoishi vijijini. Kuku hawa hufugwa huria {free-range}, yaani hufungiwa ndani nyakati za usiku na hufunguliwa asubuhi ili wajitafutie chakula.

Kuku hawa hutoa mazao machache sana yaani nyama na mayai, kwa mfano kuku mmoja hutaga kiasi cha mayai 40-60 kwa mwaka badala ya 100-150 iwapo ataimarishwa na kutunzwa vizuri. Pia uzito wa kuku hai ni wa chini sana, wastani wa kilo 1.0 – 1.5 katika umri wa zaidi ya miezi 6 badala ya kilo 1.8 – 2.5 iwapo atatunzwa vizuri.


mikoa/kanda

East Africa